Jumatatu 28 Septemba 2026 - 19:15
Simulizi za Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi kuhusu Jihadi za Sayyid Hassan Nasrullah; Je! Hizbullah iligeukaje kuwa “Mti Mwema”?

Hawza/ Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika hotuba zake mbalimbali, amemtaja Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kuwa miongoni mwa watu mashuhuri katika jihadi, ushujaa, busara na kujitolea, na kwa kuashiria nafasi yake katika kukua Hizbullah, amesisitiza kwamba utu wake, njia yake na sauti yake vitaendelea kudumu katika safu ya Muqawama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kwa kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon, Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, tunawaletea wasomi na wasomaji wapendwa matamko ya Imam Shahidi kuhusu shakhsia na juhudi za jihadi za mwanazuoni huyu mwanamapambano.

Msaada na dua kwa ajili ya mafanikio ya uongozi wa Hizbullah ya Lebanon

“Uwepo wenu [Baraza la Uongozi la Hizbullah ya Lebanon] nchini Lebanon, katika eneo hilo nyeti, ni neema kubwa sana kwa Uislamu na Umma wa Kiislamu, na tunatumaini kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu atawapa mafanikio na kuwasaidia na kuwaongoza katika yale ambayo yana ridhaa Yake...

“Mimi huwa ninawaombea dua daima, na ninaamini kwamba si mimi peke yangu; wapo wengi wanaowaombea dua na kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape mafanikio, na kwa unyenyekevu wanamuomba Mwenyezi Mungu awafanikishe katika njia yenu, bila shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu atajibu dua, na mtafanikiwa katika kazi yenu.”

03/09/1377 [24 Novemba 1998]

Uelewa wa kina; sharti la kuifahamu Hizbullah na Sayyid Hassan Nasrullah kwa usahihi

“Unapoona mtu fulani anayejidai kuwa msomi wa kisasa, kwa mfano, akitia shaka kuhusu Hizbullah ya Lebanon au Sayyid Hassan Nasrullah au jambo jingine la aina hiyo, hii inatokana na kutojua mazingira; yaani, huo ndio mtazamo wake wa matumaini zaidi, bila shaka mtu anaweza pia kuwa na mtazamo wa kukata tamaa; lakini kwa mtazamo wa matumaini, maana yake ni kwamba hajui kinachoendelea katika eneo hili, hamjui Sayyid Hassan Nasrullah ni nani, haijui Hizbullah ni nini, na haujui uhusiano wake na Iran una athari gani katika hatima ya nchi na hatima ya Mapinduzi, hii inatokana na kutokujua.

“Kwa hiyo, kuangalia mazingira ya wanafunzi, mazingira ya nchi na mazingira ya dunia kwa macho yaliyofumbuka—jambo ambalo nililiita miaka miwili au mitatu iliyopita ‘baswira’—baadhi ya watu pia walikerwa na hilo wakasema: ‘Mheshimiwa! Baseira, baseira! Kwa nini mnasema baswira?’ Naam, ni baswira; baswira maana yake ni kuangalia kwa macho yaliyofumbuka.”

12/04/1395 [02 Julai 2016]

Nafasi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah katika kubadilisha mwelekeo wa Muqawama katika eneo

“Kama watu kama Shahidi Sinwar wasingepatikana ambao walipigana hadi dakika ya mwisho, hatima ya eneo ingekuwa namna moja; lakini kwa kuwa wamepatikana, sasa iko namna nyingine.

“Kama watu wakubwa kama Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah wasingepatikana ambao waliunganisha jihadi, akili, ushujaa, kujitolea na kujitoa muhanga, na kuvipeleka vyote hivyo uwanjani, harakati ingekuwa namna moja; lakini kwa kuwa wamepatikana, harakati sasa iko namna nyingine, haya ni mambo muhimu sana.”

02/08/1403 [22 Oktoba 2024]

Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah; mbunifu wa ukuaji na nguvu ya kudumu ya Hizbullah ya Lebanon

“Sayyid wetu mpendwa amepanda hadi kwenye daraja za juu za mashahidi, na yeye mwenyewe amefikia kile alichokuwa akikitarajia, lakini pia ameacha hapa urithi wa kudumu, nao ni ‘Hizbullah’.

“Hizbullah, kwa baraka ya ushujaa wa Sayyid, busara ya Sayyid, subira yake na tawakkul yake ya ajabu, ilikua; ilikua kwa kiwango kisicho cha kawaida, na kwa hakika ikawa taasisi ambayo adui mwenye silaha na aliyeandaliwa kwa kila aina ya silaha za kimaada, za kimaneno, za propaganda, za vyombo vya habari na nyinginezo, ameshindwa kuishinda, na Inshaallah hataweza kuishinda.

“Marehemu Bwana Sayyid Hassan Nasrullah aliifanya Hizbullah kuwa kiumbe wa aina hii, kuwa jambo la aina hii.”

17/08/1403 [07 Novemba 2024]

Kuuawa kishahidi Sayyid Hassan Nasrullah; ujumbe wa kuendeleza Muqawama na kutokata tamaa 

“Sisi sote tumepatwa na msiba na tuko katika maombolezo kwa ajili ya Sayyid wetu mpendwa [Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah]. Hili ni pigo kubwa na kwa hakika limetufanya kuwa wenye maombolezo.

“Lakini maombolezo yetu hayamaanishi huzuni, kuvurugika wala kukata tamaa; ni ya aina ileile ya maombolezo ya Sayyid al-Shuhadaa Hussein bin Ali (amani iwe juu yao wawili); ni maombolezo yanayohuisha, yanayofundisha, yanayotoa msukumo na yanayozalisha matumaini.

“Sayyid Hassan Nasrullah mwili wake umeondoka miongoni mwetu, lakini shakhsia yake halisi, roho yake, njia yake na sauti yake yenye nguvu bado ipo miongoni mwetu na itaendelea kuwepo. Alikuwa bendera iliyoinuliwa juu ya Muqawama dhidi ya mashetani madhalimu na wanyang’anyi; alikuwa ulimi uliozungumza kwa uwazi na mtetezi shujaa wa waliodhulumiwa; alikuwa chanzo cha kuwapa moyo na ujasiri wapiganaji na wanaodai haki.

“Upeo wa umaarufu na athari yake ulikuwa umevuka Lebanon, Iran na nchi za Kiarabu; na sasa kuuwawa kwake kishahidi kutaongeza athari hiyo.

“Ujumbe wake muhimu zaidi wa maneno na vitendo katika maisha yake ya duniani kwa ajili yenu enyi taifa waaminifu la Lebanon, ulikuwa kwamba; kwa kuwapoteza watu mashuhuri kama Imam Musa al-Sadr, Sayyid Abbas Musawi na wengine, msikate tamaa wala kuvurugika; msitie shaka katika njia ya mapambano; ongezeni juhudi na uwezo wenu; zidisheni mshikamano wenu; na mkabiliane na adui mvamizi na mchokozi kwa kuimarisha imani na tawakkul, na mumfanye ashindwe.

“Wapendwa wangu! Enyi wananchi waaminifu wa Lebanon! Enyi vijana wenye hamasa wa Hizbullah na Amal! Enyi wanangu! Leo pia, matakwa ya Sayyid wetu Shahidi kwa taifa lake, kwa safu ya Muqawama na kwa Umma wote wa Kiislamu ni hayahaya.

“Adui mwovu na dhaifu, kwa kuwa hawezi kuzipiga pigo kubwa taasisi imara za Hizbullah, Hamas, Jihad ya Kiislamu na mashirika mengine ya wapiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu, anahesabu mauaji ya kisiasa, uharibifu, ulipuaji wa mabomu, mauaji ya raia na kuwafanya watu wasio na silaha kuwa waombolezaji kuwa ni ishara ya ushindi wake.

“Matokeo ni nini? Matokeo ya tabia hii ni kuongezeka hasira, kuongezeka hamasa ya wananchi, kujitokeza wanaume, makamanda, viongozi na watu wengi zaidi wanaojitolea nafsi zao, kukaza zaidi mzingiro dhidi ya mbwa mwitu huyo mwenye kiu ya damu, na hatimaye kuondolewa uwepo wake wenye aibu Inshaallah.”

13/07/1403 [04 Oktoba 2024]

Sayyid Hassan Nasrullah; mbunifu wa ukuaji wa taratibu na nguvu ya Hizbullah ya Lebanon katika mapambano

“Sayyid mpendwa [Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah] alikaa kwa miaka thelathini akiongoza mapambano magumu; aliikuza Hizbullah hatua kwa hatua:

﴿کَزَرْعٍ أَخْرَجَ شَطْأَهُ فَآزَرَهُ فَاسْتَغْلَظَ فَاسْتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِ یُعْجِبُ الزُّرَّاعَ لِیَغِیظَ بِهِمُ الْکُفَّارَ وَعَدَ اللَّهُ الَّذِینَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِنْهُمْ مَغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِیمًا﴾

“Ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, likawa nene, likasimama juu ya shina lake na kuwafurahisha wakulima, ili kwao awaghadhabishe makafiri, Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini na wakatenda mema miongoni mwao msamaha na malipo makubwa.”

“Kwa busara ya Sayyid, Hizbullah ilikua hatua kwa hatua, kwa subira, kwa mantiki na kwa njia ya kawaida, na ikaonesha matokeo ya uwepo wake katika vipindi mbalimbali kwa kuurudisha nyuma utawala wa Kizayuni:

﴿تُؤْتِی أُکُلَهَا کُلَّ حِینٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا﴾

‘Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake.’ “Hizbullah kwa hakika ni ‘Mti Mwema’.

“Hizbullah na kiongozi wake shujaa na shahidi ni kiini cha fadhila za kihistoria na utambulisho wa Lebanon.”

13/07/1403 [04 Oktoba 2024]

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha